Home Images
Karibu Fresh Spring Fellowship Church
(Ngome ya Yesu)
Kimara Temboni - Dar-es-Salaam, Tanzania.
Mwanzo
Fresh Spring Fellowship Church ilianza Mwezi wa Oktoba 2017 na Mbeba maono Kuhani na Mwalimu Musa Richard Mwacha ambaye alianza kumtumikia Mungu tangu miaka ya 90.
Maono na Malengo
Maono na malengo ya “Fresh Spring Fellowship Church” Ngome ya Yesu, chini ya mbeba maono, Kuhani Musa Richard Mwacha ni Kuhubiri na kueneza Injili sahihi ya kitume; Kuwainua waumini katika Uombaji; uamini katika Wokovu;Kuwafungua waliofungwa katika itikadi za Kidini na Madhehebu; na Kuwafungua na kuwaponya wote waliofungwa na kukandamizwa na shetani.
Maono na Malengo
Maono na malengo ya “Fresh Spring Fellowship Church” Ngome ya Yesu, chini ya mbeba maono, Kuhani Musa Richard Mwacha ni Kuhubiri na kueneza Injili sahihi ya kitume; Kuwainua waumini katika Uombaji; uamini katika Wokovu;Kuwafungua waliofungwa katika itikadi za Kidini na Madhehebu; na Kuwafungua na kuwaponya wote waliofungwa na kukandamizwa na shetani.
Kuhani Richard Mwacha
Maono na malengo ya “Fresh Spring Fellowship Church” Ngome ya Yesu, chini ya mbeba maono, Kuhani Musa Richard Mwacha ni:
- Kuhubiri na kueneza Injili sahihi ya kitume, inayoamini:
- Kwamba Mungu ni Mmoja tu ambaye Jina lake ni Yesu Kristo.
- Ubatizo wa maji mengi katika Jina la Yesu Kristo
- Kuwainua waumini katika Uombaji (Maombi); Ili kutengeneza Jeshi mahiri la Yesu Kristo.
- Kuwa mwumini wa “Fresh Spring Fellowship Church” Ngome ya Yesu; ni lazima uamini katika Wokovu. Ndiyo maana lengo mojawapo ni kuwafundisha na kuwainua waumini katika Wokovu.
- Kuwafungua waliofungwa katika itikadi za Kidini na Madhehebu. Aidha “Fresh spring fellowship church” Ngome ya Yesu, hupokea mtu yeyote bila kujali Dini au Dhehebu lake.
- Kuwafungua na kuwaponya wote waliofungwa na kukandamizwa na shetani kupitia nguvu za giza (Uchawi n.k).
News
-
Madhimisho ya Siku ya wanawake duniani 2023 "Fresh Spring Fellowship"
SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2023 JINSI ILIVYO ADHIMISHWA FRESH SPRING FELLOWSHIP (NGOME YA YESU) KWA KUHANI MUSA RICHARD MWACHA. MAHUSIANO…
Read More -
Ibada Jumapili 26-March-2023 (KUREJESHA UWEZO WAKO ULIOPOTEA)
KUREJESHA UWEZO WAKO ULIOPOTEA Mwanadamu Mungu amemuumba na sehemu tatu ambazo ni MWILI, NAFSI na ROHO. Na kwa kawaida hivi…
Read More -
Ibada Jumapili 9 April 2023 (SOTE TUTAFANANA NA MALAIKA)
IBADA YA KUPOKEA MWILI NA DAMU YA YESU SOTE TUTAFANANA NA MALAIKA Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke ana sura mbili. Sura…
Read More
- 1
- 2
Ibada
Ibada za Fresh Spring Fellowship Church (Ngome ya Yesu), Kimara Temboni zipo siku tatu katika wiki.
- Jumapili Kuna Ibada mbili, Ibada ya kwanza inaanza saa 12.00 (Saa Kumi na mbili) Asubuhi, na Ibada ya pili inaanza saa 11.00 (Kumi na Moja) jioni.
- Siku za Jumanne na Ijumaa ibada zinaanza saa 9.00 (Tisa) Alasiri.
Sadaka
Sadaka ni njia mojawapo ya kujiunganisha na Mungu, kwa Imani. Fresh Spring Fellowship (Ngome ya Yesu) tuna sadaka za aina sita (6). Nazo ni Sadaka ya Ufungulivu, Sadaka ya Karama na Vipawa, Sadaka ya kuinuliwa, Zaka au Fungu la kumi, Sadaka ya shukurani na Partnership.
Maombi
Huduma ya Maombi kwa mtu binafsi hupatikana kupitia njia nne. Nazo ni kupitia kwa simu, kwa mitandao, kupitia kujaza fomu maalumu pale Mapokezi “Fesh Spring Fellowship Church” an kusoma kitabu kilichoandinkwa na Kuhani na Mwalimu Musa Richard Mwacha kiitwacho “Maombi ya Ufungulivu”.